Matumaini yangu wapendwa wangu ni wazima, wale ambao hali zao si njema Mungu awatangulie awape uzima, Amen. Mada ya leo, tunaanza kuzungumzia suala la nyumba. Nyumba ni kitu ambacho binadamu yeyote anahitaji ili aishi. Wakati wa ujenzi wa nyumba inabidi vitu mbali mbali vizingatiwe, na cha kwanza ni sebule. Sebule ni eneo ambalo mtu yeyote anapaona hasa wageni wetu. Na ni kitu cha kwanza mgeni yeyote anakiona hivyo inabidi parembwe haswa. Wakati wa kutengeneza hakikisha unatengeneza kulingana na familia yako. Kama tayari una watoto na ni wakubwa nina imani utunzaji utakua mkubwa, tofauti na mtu mwenye familia iliyo na watoto wadogo lazima azingatie vitu vingi. Kama una watoto wakubwa unaweza kuamua uweke makochi yenye rangi ya maziwa kama inavyoonekana na ukaweka mapambo ya vitu vya kuvunjika.
Kama una familia ya watoto wadogo ni vizuri ukaweka makochi na hata rangi za ukutani zikawa zile rangi zisizoonyesha sana uchafu kwa sababu ya watoto.ambao ni rahisi kuchafua kama ukiweka makochi yenye rangi nyeupe. Rangi zinazofaa sana kama una watoto wadogo ni kahawia inaweza kua iliyokolea au isiyokolea. Nyeusi haipendezi sana kwa sebule kwa sababu inapoa sana na inaweza kuonekana giza wakati fulani. Angalia mfano hapa chini.
No comments:
Post a Comment