Leo ni wakati mwingine matumaini yangu wote wazima wapendwa. Leo bado tutaendelea kuona suala la harusi. Mada ya leo itahusu mapambo ya bibi harusi ambayo ni cheni, hereni na bangili. Wakati wa kuchagua mapambo haya inabidi kuzingatia ubora ili kuepuka kuharibikiwa navyo siku yenyewe. Pia inabidi kuchagua vitu vya kawaida tu ambavyo vitakua na mvuto wa kipekee kuliko vingi ambavyo havitapendeza. Mfano mdada wetu hapo chini kachagua cheni ya duara iliyotosha shingoni vizuri.
Au pia kama wewe ni mpenzi wa cheni ambazo zinashuka yaani hazikai shingoni kama mduara, hakikisha unafanya chaguo zuri kulingana na pendekezo lako. Angalia picha chini jinsi cheni inavyoweza kukaa.
Kwa upande wa hereni, wakati unachagua, angalia namna jinsi shingo yako ilivyo na hereni unayotaka kuvaa. Kama huna shingo ndefu, mara nyingi inapendeza sana kuvaa hereni ambazo si ndefu sana kwa sababu kupendeza na hereni, lazima ionekane vizuri na ionekane umeivaa na inaning'inia au wenyewe huziita drop-earings kama si ndefu basi imetosha kwenye sikio. Angalia picha jinsi hereni inavyokaa..
Tunamalizia mada yetu na urembo wa mikono maarufu kama bangili. Kila kitu kikizidi kina madhara yake. Bangili kwa bibi harusi zinatakiwa moja au mbili ikizidi kuna wasi wasi isilete picha nzuri sana. Mfano wa urembo huu ni kama unavyoonekana kwenye picha.
No comments:
Post a Comment