Kipengele cha kwanza nilichopenda kuanzia ni kuhusu suala zima la harusi. Harusi kama wengi tunavyojua ni jambo la kheri hivyo inabidi kuhakikisha wahusika kwenye harusi yaani Bwana na Bibi harusi wanapendeza. Wengine hupenda kuweka utofauti mfano wenzetu Nigeria hupenda kuvaa nguo za asili. hii nayo ni sawa ilimradi wamepambwa vizuri na wamependeza. Mfano picha hapo chini inaonyesha harusi mojawapo ya nchini Nigeria ambapo wamechanganya utamaduni wao na usasa kidogo kama umuonavyo bibi harusi hapo chini.
Kwa kuanza suala zima la harusi, nitaanzia na mavazi, hasa ya wakina dada yaani magauni ya bibi harusi. Mdada ambaye anaolewa hivi karibuni na hajui achague gauni lipi pengine ameshaenda maduka mengi, kashajaribu mpaka wauzaji wamechoka, cha kwanza zingatia mwili wako ulivyo, yaani chagua gauni kulingana na wewe mwenyewe, usivae gauni tu kwa sababu ulienda kwenye sherehe ya shosti ukakuta kavaa gauni zuri na wewe ukataka kama hilo kumbe halitokukaa vzuri. Mfano angalia picha chini ya mdada aliyependeza na gauni lake.

Vile vile wakati wa uchaguzi wa gauni angalia na uhuru utakaokua nao. Mwingine hayuko huru kuvaa gauni litakaloacha mabega wazi ila anaona harusi fulani mtu alivaa gauni la mabega wazi likampendeza na yeye anaona bora avae gauni kama hilo ila isije inafika siku yenyewe unaona aibu sana, unashindwa kujiachia na kujiziba ziba. Kama huwezi kuacha mabega wazi kuna aina mbali mbali za uvaaji unaweza kuamua kuvaa kikoti na bado ukapendeza. Mfano picha hapo chini mdada huyo anaonekana kufurahia uvaaji wake.
No comments:
Post a Comment