Kwa mara nyingine, tunakutana tena na mambo ya sebule zetu. Hii hasa kwa wakina mama na hata wadada. Mapambo ya sebuleni hayatakiwi kuwa mengi. Mfano picha za wanafamilia, maua na mapambo mengine machache. Sebule haitakiwi kuwa imesheheni vitu vingi kupindukia mpaka ikajaa. Vitu vichache tu vinatosha. Mfano picha, maua, kutakuwa na tv na radio na mengineyo yasiyozidi kupindukia.
Wakati wa upambaji pia zingatia rangi utakazotumia. Rangi nyeusi kila kitu mara nyingi hua haina mvuto sana. Kuna rangi mbali mbali zenye mvuto wake kulingana na aina ya mapambo na namna unavyopangilia vitu vyako. Mfano rangi kama kahawia, rangi ya machungwa na nyinginezo.
Rembuka
Jifunze aina mbali mbali za mavazi, nywele, urembo wa harusi na mitindo mbali mbali ya kuremba nyumba na mitindo tofauti tofauti ya maisha.
Wednesday, 30 April 2014
PENDA UNAPOISHI.
Matumaini yangu wapendwa wangu ni wazima, wale ambao hali zao si njema Mungu awatangulie awape uzima, Amen. Mada ya leo, tunaanza kuzungumzia suala la nyumba. Nyumba ni kitu ambacho binadamu yeyote anahitaji ili aishi. Wakati wa ujenzi wa nyumba inabidi vitu mbali mbali vizingatiwe, na cha kwanza ni sebule. Sebule ni eneo ambalo mtu yeyote anapaona hasa wageni wetu. Na ni kitu cha kwanza mgeni yeyote anakiona hivyo inabidi parembwe haswa. Wakati wa kutengeneza hakikisha unatengeneza kulingana na familia yako. Kama tayari una watoto na ni wakubwa nina imani utunzaji utakua mkubwa, tofauti na mtu mwenye familia iliyo na watoto wadogo lazima azingatie vitu vingi. Kama una watoto wakubwa unaweza kuamua uweke makochi yenye rangi ya maziwa kama inavyoonekana na ukaweka mapambo ya vitu vya kuvunjika.
Kama una familia ya watoto wadogo ni vizuri ukaweka makochi na hata rangi za ukutani zikawa zile rangi zisizoonyesha sana uchafu kwa sababu ya watoto.ambao ni rahisi kuchafua kama ukiweka makochi yenye rangi nyeupe. Rangi zinazofaa sana kama una watoto wadogo ni kahawia inaweza kua iliyokolea au isiyokolea. Nyeusi haipendezi sana kwa sebule kwa sababu inapoa sana na inaweza kuonekana giza wakati fulani. Angalia mfano hapa chini.
VIATU VYA BIBI HARUSI
Kwa mara nyingine tunakutana tena katika eneo letu kwa mada nyingine lakini bado tutazungumzia suala la harusi. Leo tutazungumzia mambo ya viatu. Mimi mwenyewe kiatu ni kitu muhimu kwangu. Raha ya kiatu kikutoshe vizuri yaani kisikubane wala kukuzidi hata kidogo. Kama wewe si mpenzi wa mchuchumio mrefu kama kwenye picha hapo chini basi ni heri ukavaa aina tofauti ya kiatu, wazungu wenyewe huita "wedge". Ni muhimu kuvaa kiatu kinachotosha kama tujuavyo sherehe itakubidi Bibi harusi ucheze na waalikwa wako na siku hizi kuna kitu cha Kwaito sasa afadhali uvae kitu utakachokua huru nacho na kitakachokutosha.
Kwa wale wenzangu na mimi msioweza mchuchumio wa ncha, wanamitindo hawakuwaacha nyuma, mkashindwa kuserebuka kwenye harusi zenu. Kuna viatu ambavyo ni vyepesi na rahisi kutumiwa na mvaaji yeyote. Viatu hivi wenzetu huviita "wedge". hivi ni viatu ambavyo mtu yeyote huweza kuvaa na kumpa uhuru mvaaji.
Kwa wale wenzangu na mimi msioweza mchuchumio wa ncha, wanamitindo hawakuwaacha nyuma, mkashindwa kuserebuka kwenye harusi zenu. Kuna viatu ambavyo ni vyepesi na rahisi kutumiwa na mvaaji yeyote. Viatu hivi wenzetu huviita "wedge". hivi ni viatu ambavyo mtu yeyote huweza kuvaa na kumpa uhuru mvaaji.
UREMBO WA HARUSI.
Leo ni wakati mwingine matumaini yangu wote wazima wapendwa. Leo bado tutaendelea kuona suala la harusi. Mada ya leo itahusu mapambo ya bibi harusi ambayo ni cheni, hereni na bangili. Wakati wa kuchagua mapambo haya inabidi kuzingatia ubora ili kuepuka kuharibikiwa navyo siku yenyewe. Pia inabidi kuchagua vitu vya kawaida tu ambavyo vitakua na mvuto wa kipekee kuliko vingi ambavyo havitapendeza. Mfano mdada wetu hapo chini kachagua cheni ya duara iliyotosha shingoni vizuri.
Au pia kama wewe ni mpenzi wa cheni ambazo zinashuka yaani hazikai shingoni kama mduara, hakikisha unafanya chaguo zuri kulingana na pendekezo lako. Angalia picha chini jinsi cheni inavyoweza kukaa.
Kwa upande wa hereni, wakati unachagua, angalia namna jinsi shingo yako ilivyo na hereni unayotaka kuvaa. Kama huna shingo ndefu, mara nyingi inapendeza sana kuvaa hereni ambazo si ndefu sana kwa sababu kupendeza na hereni, lazima ionekane vizuri na ionekane umeivaa na inaning'inia au wenyewe huziita drop-earings kama si ndefu basi imetosha kwenye sikio. Angalia picha jinsi hereni inavyokaa..
Tunamalizia mada yetu na urembo wa mikono maarufu kama bangili. Kila kitu kikizidi kina madhara yake. Bangili kwa bibi harusi zinatakiwa moja au mbili ikizidi kuna wasi wasi isilete picha nzuri sana. Mfano wa urembo huu ni kama unavyoonekana kwenye picha.
Tuesday, 29 April 2014
HARUSI NA MAPAMBO YAKE.
Kipengele cha kwanza nilichopenda kuanzia ni kuhusu suala zima la harusi. Harusi kama wengi tunavyojua ni jambo la kheri hivyo inabidi kuhakikisha wahusika kwenye harusi yaani Bwana na Bibi harusi wanapendeza. Wengine hupenda kuweka utofauti mfano wenzetu Nigeria hupenda kuvaa nguo za asili. hii nayo ni sawa ilimradi wamepambwa vizuri na wamependeza. Mfano picha hapo chini inaonyesha harusi mojawapo ya nchini Nigeria ambapo wamechanganya utamaduni wao na usasa kidogo kama umuonavyo bibi harusi hapo chini.
Kwa kuanza suala zima la harusi, nitaanzia na mavazi, hasa ya wakina dada yaani magauni ya bibi harusi. Mdada ambaye anaolewa hivi karibuni na hajui achague gauni lipi pengine ameshaenda maduka mengi, kashajaribu mpaka wauzaji wamechoka, cha kwanza zingatia mwili wako ulivyo, yaani chagua gauni kulingana na wewe mwenyewe, usivae gauni tu kwa sababu ulienda kwenye sherehe ya shosti ukakuta kavaa gauni zuri na wewe ukataka kama hilo kumbe halitokukaa vzuri. Mfano angalia picha chini ya mdada aliyependeza na gauni lake.

Vile vile wakati wa uchaguzi wa gauni angalia na uhuru utakaokua nao. Mwingine hayuko huru kuvaa gauni litakaloacha mabega wazi ila anaona harusi fulani mtu alivaa gauni la mabega wazi likampendeza na yeye anaona bora avae gauni kama hilo ila isije inafika siku yenyewe unaona aibu sana, unashindwa kujiachia na kujiziba ziba. Kama huwezi kuacha mabega wazi kuna aina mbali mbali za uvaaji unaweza kuamua kuvaa kikoti na bado ukapendeza. Mfano picha hapo chini mdada huyo anaonekana kufurahia uvaaji wake.
Subscribe to:
Posts (Atom)